Malaika Wangu, Shujaa Wangu

0
2027

Nilishika mimba mwezi june 2013. Ilipofika mwezi wa tisa mwishoni nikaenda hospitali kufanya ultra sound ya kwanza na kuanza rasmi clinic. Daktari wangu akaona kwamba tumbo langu ni kubwa kuliko umri wa mimba. Nilipoenda kwenye ultra sound nikagundulika kwamba nina mimba ya mapacha.

Mimba yangu haikua na matatizo zaidi ya kwamba nilitapika kwa muda wote niliokua na mimba hakukua na tatizo lingine. Nilikua nimeambiwa kwamba tarehe yangu ya kujifungua itakua 24 march 2014. Lakini alfajiri ya tarehe 1 Januari 2014 siku ya mwaka mpya nikagindua kuna majimaji yananitoka. Nikaenda kanisani halafu nikaenda hospitali, hakukua na specialist siku hiyo kwavile ilikua sikuu. Kesho yake nikaamua kwenda AgaKhan hospital, nilipofika nokaambiwa kwamba yale maji ni amniotic fluid (yale majimaji yanayomzunguka mtoto tumboni) nikawekwa mapumziko nilikaa hospitali kwa wiki mbili nikiwa kwenye complete bedrest.

Tarehe 13 Januari 2014 nikiwa na mimba ya miezi sita na wiki tatu asubuhi nikaanza kujiskia maumivu kama kichomi. Daktari akaja akanipima akasema njia yangu imeanza kufunguka. Daktari wangu alitaka nijifungue kwa operation lakini mkuu wa kitengo cha gyno alisisitiza nijifunguekawaida. Mnamo saa tano usiku (11:20pm) mwanangu Estefan Victory alizaliwa. Nilimskia analia kwa nguvu nikajua yupo vizuri, baada ya dadika chache mtoto mwingine akaanza kutoka, lakini alitanguliza mikono, Daktari aliekua zamu akasema niachwe apigiwe simu specialist wangu ndio aje aendelee kunizalisha. Walimuacha mwanangu amenasa pale pale, daktari alipokuja nikapelekwa kwenye operation lakini binti yangu Aneesa Victory alishafariki.

… alitoka mtoto wa kwanza, Estefan; nilimskia analia kwa nguvu nikajua yupo vizuri. Baada ya dadika chache mtoto mwingine akaanza kutoka, lakini alitanguliza mikono, Daktari aliekua zamu akasema niachwe apigiwe simu specialist wangu ndio aje aendelee kunizalisha!

Kesho yake asubuhi nikaamka na uchungu rohoni na maumivu ya mwili. Lakini nikataka nionyeshwe mwanangu. Nikaenda chumba cha watoto nikamkuta yupo kwenye incubator, amelala amewekewa drip ya glucose na nyingine ya antibiotics. Madaktari wakaniambiwa amewekewa antibiotics kwasababu mfuko ulikua unavuja ni wake na sio wa pacha wake kwahiyo ni ilikua ni rahisi sana kwake kupata infection lakini pia watoto prematures wanaweza kupata infections kwa urahisi sana. Pamoja na kwamba alikua amezaliwa mapema sana alikua anapumua mwenyewe bila mashine za oksijeni.

Baada ya hapo tulikaa hospitali wiki mbili, mwanangu akiwa kwenye incubator akiwa anafundishwa kunywa maziwa yangu, alianza kunyweshewa kwenye mrija uliokua puani, na baadae kidogokidogo akaanza kunyweshwa na kikombe mdomoni. Wiki moja baada ya kujifungua nikawa napatwa na homa kali sana, usiku mmoja nikaamka nikiwa navuja damu zimelowesha kitanda kutoea eneo lile la mshono, ikabidi madakrati waje usiku wafungue wanikamue damu ile chafu itoke. Kesho yake asubuhi nikarudishwa theatre nikafunguliwa na mishipa iliyokua inavuja ikaziba. Muda huo wote sikuweza kumuhudumia mwanangu ipasavyo. Lakini niliendelea kupump maziwa hadi nilivyoamka tu kutoka theatre. Estefan aliendelea vizuri baada ya wiki mbili tangu azaliwe tukaruhusiwa, tuliruhusiwa akiwa na uzito wa kilo 1.56kg.

Tulivyofika nyumbani akwa anaendelea vizuri. Lakini alipofunga mwezi na nusu akaanza kutapika kila anapolishwa. Madaktari wake wakasema ana kitu kinaitwa reflux na ni common sana kwa premature babies. Hali ile ikaendelea na kwa siku alikua anaweza kutapika hadi mara sita. Alikua hajui kunyonya kwahiyo maziwa yote nilikua napump mwenyewe. Alipokua na miezi mitatu hivi akaumwa pneumonia, hali ya kutapika ikazidi kua mbaya. Kwahiyo kumlisha ilikua ni kazi ya masaa 24. Muda wote huo hakuwahi kushuka uzito ulikua unapanda tu, kwasababu kila akitapika alikua anarudishiwa.

Hali ya kutapika iliendelea hadi akiwa na na mwaka, mwezi wa pili mwaka huu 2015 na juu ya hapo alikua hapendi kula kabisa kabisa. Nikashauriwa nimpe juice fulani ya aloevera na supplements za vitamins za watoto, kwa mijuiza ya mungu ile hali ikakata ghafla hadi sasa hivi. Leo hii May 2015 Estefan ana kilo 11kg, anatambaa na kusimamia vitu, ana akili na ni mtoto mchangamfu sana na mjanja. Kwa shida zote alizozipata na maumivu yote aliyoyapata mwanangu ameyashinda na anasonga mbele. Mwanangu ni shujaa, alipigana kuishi. Pamoja na kwamba nilipoteza mtoto mwingine Estefan amejaza nafasi yote moyoni mwanangu. Sikuwahi kujua furaha na faraja ninayoipata kila nikiwa na mwanangu. Jina lake la katikati ni Victory maana yake ni ushindi. Kwasababu mungu wetu alitushindia hili. ~ Matilda
Mke wangu alipoanza kuumwa niliogopa sana. Nilikua nimeskia stori nyingi jinsi uzazi unavyoweza kusababisha kifo. Akiwa hospitalini muda wote mimi sikuweza kufanya jambo lolote. Ofisini kwangu walinipa likizo fupi ili nimuhudumie mke wangu. Siku amezaliwa Estefan ilianza tu vizuri. Nilipofika hospitali nikaambiwa kwamba inabidi mke wangu ajifungue siku hiyo. Nilijua ni kiasi gani tulikua tumepigania watoto wetu. Nilipoambiwa kwamba binti yetu amefariki nilisikitika sana na sikujua nitamweleza vipi mke wangu habari hizo. Nilienda kumuona mwanangu Estefan alipozaliwa. Alikua amewekewa mirija mingi na oksijen. Pamoja na hayo yote moyo wangu ulijawa na furaha kwamba na mimi nilikua baba. Siku zilikua hazosongi, kiukweli nilikua silali na nilikua na msongo wa mawazo na wasiwasi muda wote. Madaktari walituambia kabisa mara nyingine watoto premature huwa wanakufa kwa kusahau kupumua, nilichanganyikiwa, namshukuru mungu kwa kututia ujasiri mimi na mke wangu.

Katika yote tuliyopitia ambayo mengi ameyaelezea Matty, namshukuru mungu kwa jambo moja tu kwamba katika yote hayo alikua pamoja na sisi. Nampenda mwanangu kuliko ninavyoweza kuelezea, ananipa sababu ya kufanya kazi kwa bidii na kuweza kumpatia only the best in this world. Alichagua kuishi hivyo basi as long as I live nitahahakisha kwa kadri ya uwezo wangu anaishi maisha bora kabisa. He is my Hero
~ Edgar

LEAVE A REPLY