Mitindo ya Kusuka kwa watoto

0
30364

Nywele ndefu ni nzuri kwa watoto wa kike, wazazi wengine hupendelea kuwanyoa watoto wao wakati wazazi wengine hupendelea kuwasuka watoto. Vyote viwili (kusuka au kunyoa) ni mapenzi ya wazazi na utulivu wa watoto.

Kwa mtoto anayependa kusuka ni vyema akasuka mara moja kwa wiki au kwa wiki mbili,hii inategemea na aina yamsuko atakaosukwa. Kwa mfano kama mtoto atasukwa nywele za kawaida bila kuongezea kitu chochote ni vyema akasukwa maramoja kwa wiki. Yaani jumapili baada ya kuoshwa nywele vizuri na kukaushwa ili mtoto asipate muwasho.

MITINDO YA KUSUKA WATOTO
Kuna aina nyingi za mitindo ya nywele. Kuna kusuka kwa kutumia uzi au rasta au kusuka nywele zakawaida bila kuongeza kitu chochote. “Aina gani mtoto asuke” inategemea na mapenzi ya mzazi. Watoto wengi hupenda kusuka kwa kuchanganya na uzi, staili hii ni nzuri na huwapendeza sana watoto japo katika usukaji msusi hatakiwi kuacha mikia iwe mirefu sana kiasi ambacho itamsumbua mtoto anapokuwa anacheza au anakula au hata anapokuwa darasani.

Inashauriwa kua Urefu wa mikia ya nywele inatakiwa kuishia mwisho wa sikio. Rasta nazo ni nzuri lakini si sana kama uzi kwani rasta huchomoka (nyuzinyuzi) ambazo ni hatarishi kwa afya ya mtoto. Pia mtoto hatakiwi kusukwa nywele nyingi yaani zitakazojaza kichwa mpaka akashindwa kulala au kucheza. Mfano endapo mtoto anasuka kwa kutumia uzi, msusi asitumie Zaidi ya bunda mbili za uzi. Baada ya kusuka msusi anaweza ongeza urembo kwa juu, mfano shanga za rangi mbalimbali au  vibanio vya nywele vya kitoto.

Tusiwaweke Watoto Wetu Dawa Za Nywele, Tuwatafutie Mitindo Mizuri Ya Kusuka Na Watapendeza Sana

Endapo mzazi ataamua mtoto asukwe nywele za kawaida yaani bila kuchanganya na kitu chochote ni vizuri mtoto akasukwa kwa umaridadi na nywele ambazo zitaweza kukaa wiki nzima bila kufumuka na kumfanya mtoto aonekane nadhifu wiki nzima.

 

LEAVE A REPLY