Lishe kwa watoto wa siku moja mpaka miezi sita

3
24037

Lishe kwa watoto

Kufanya maamuzi maalum juu ya lishe ya mwanao ni kitu muhimu sana. Lishe bora ni muhimu sana na wadau wengi wa afya ya watoto ikowemo shirika la chakula duniani (WHO) wanasisitiza na kuhamasisha wazazi kufikiria kuhusu maamuzi watakayofanya juu ya lishe ya watoto wao kama maamuzi ya afya. Msingi wa afya bora huchangiwa na lishe bora kwanzia mimba.

photogrid_1478200625325

Wakati wa Mimba:

Kabla ya mimba mama anatakiwa ajiandae kwaaji ya kubeba ujauzito, kwa mfano mwanamke ambaye atabeba mimba akiwa na upungufu wa asidi ya foliki anaweza kupata mtoto mwenye mgongo wazi. Vyakula vyenye aside ya folik kwa wingi ni mboga za majani za kijani, matunda kama machungwa, maharage, nafaka zisizo kobolewa nk.

Mama mjamzito anatakiwa azingatie misingi ya lishe bora ili aweze kujipatia virutubisho vya kutosha kwa ajili yake na ya mtoto aliyeko tumboni mwake. Lishe bora huzingatia mchanganyiko wa vyakula mbalimbali, kiasi sahihi, ukamilifu wa virutubisho na kwa wakati sahihi. Zaidi ya hayo kuna ongezeko la uhitaji wa virutubisho vifuatavyo mfano protein, madini ya chuma, kalsiam na asidi ya folik. Hivyo vyakula (nyama, samaki, mayai, vyakula vya jamii ya maharage, kokwa na mbegu mbegu, mboga za majani za kijani, maziwa na bidhaa zake, matunda na mboga mboga kwa ujumla) vyenye virutubisho twajwa hapo juu vinatakiwa viliwe kwa wingi ili kuhakikisha afya ya mama na mtoto atakaye zaliwa.

Mfano wa ratiba ya chakula wakati wa mimba

Kifungua kinywa

01 – 02 asubuhi

Asusa ya asubuhi

04 – 05 asubuhi

Chakula cha mchana

07 – 08 mchana

Asusa ya jioni

10 – 11 jioni

Chakula cha usiku

01 – 02 usiku

-maziwa

-mihogo/viazi vitamu

-kachumbari

-ndizi mbivu

-maji ya kunywa

-Bakuli la matunda

Au

-Juice ya maembe na beetroot

-karanga vijiko 2

-Ugali wa dona

-Maharage/dagaa

-Majani ya maboga

-embe/tikiti/papai

-Maji ya kunywa

-Glass ya mtindi

Au

Chai

Yai la kuchemsha

Mkate kipande 1

-Wali

-Maharage/nyama

-Majani ya maboga

-Chungwa/nanasi

-Maji ya kunywa


Lishe kwa watoto wa 0 mpaka miezi 6

Katika kipindi cha miezi sita ya kwanza wataalamu wanashauri mtoto atumie maziwa ya mama tu bila kuchanga na kitu chochote hata maji. Maziwa ya mama yana virutubisho vyote anavyohitaji mtoto mchanga katika uwiano sahihi, hivyo hufanya maziwa ya mama yawe ni chakula bora na sahihi kwa mtoto mchanga kuliko maziwa mengine yoyote.  Hata kama mama anakwenda kazini, ni vizuri akikamua maziwa na kumwachia mwanae. Maziwa yakiwekwa kwenye joto la kawaida (room temperature) yanaweza kukaa masaa manne mpaka sita, yakiwekwa kwa jokofu hukaa mpaka siku tatu, yakikaa katika freezer hukaa kati ya miezi sita mpaka mwaka inategemee ubaridi wa freezer lenyewe.

photogrid_1478201873262

Faida za maziwa ya mama

Maziwa ya mama yana kinga mwili hasa yale maziwa ya mwanzo

Maziwa ya mama humkinga mtoto na maambukizi na magonjwa mabilimbali

Maziwa ya mama husaidia ukuaji muafaka wa ubongo hivyo mtoto kuwa na upeo mkubwa

Maziwa ya mama ni safi na salama kwa mtoto wakati wote

Maziwa ya mama hupatikana kwa urahisi na haya gharama

Maziwa ya mama yana joto sawia na joto la tumbo la mtoto hivyo hayawezi kudhuru utumbo wa mtoto.

Maziwa ya mama huzuia tatizo la kukosa choo kwa watoto

Unyonyeshaji unasaidia pia kuongeza mapenzi kati ya mama na mtoto.

Mama anayenyonyesha vizuri anaweza kujikinga na magonjwa mfano saratani ya matiti na kizazi

Mama anayenyonyesha vizuri anaweza kurudi  katika uzito wake  wa kabla ya ujauzito

Uzalishaji wa maziwa

Wanawake huweza kutoa maziwa baada ya kujifungua chini ya ushawishi wa homoni za prolaktini na okistosini. maziwa ya kwanza kutolewa hujulikana kama kolostramu, ambayo huwa na kiwango cha juu cha imunoglobuliniIgA ambayo huzingira njia ya utumbo. Hii husaidia kulinda mtoto mchanga mpaka mfumo wa kinga yake unafanya kazi vizuri, na inajenga athari ya kupumzika, huondoa mekoniamu (choo cheusi cha kwanza cha mtoto) na kusaidia kuzuia kujengwa upya kwa bilirubini (sababu muhimu ambayo huchanjia ugonjwa wa macho kugeuka manjano).

Kuna sababu nyingi kwa nini mama hawezi kutoa maziwa ya kutosha. Baadhi ya sababu  ni kama ifuatavyo

Maswala ya kuridhi (katika familia hawana uwezo mkubwa wa kuzalisha maziwa) asilimia ndogo ya  wamama wenye shida hii

Kushindwa kumuunganisha mtoto vizuri kwenye titi

Kutokujiandaa kisaikolojia kwaajili ya kumnyonyesha mtoto wako.

Ukosefu wa chakula au kupungukiwa na maji mwilini

Kutonyonyesha mara kwa mara

Maumivu, ugonjwa au matumizi ya dawa fulani zikiwemo dawa za uzazi wa mpango

Sonona na msongo wa mawazo

Jinsi ya kuongeza uzalishaji wa maziwa ya mama

Maandalizi ya kisaikolojia juu ya kunyonyesha mtoto wako kabla ya kujifungua

Kula chakula cha kutosha na hasa vimiminika mfano supu, juisi halisi na chai mfano chai ya mchaichai, chai ya mlonge, soya nk. ispokuwa (green tea, chai ya rangi na kahawa) hazishauriwi

Nyonyesha mara nyingi iwezekanavyo au kamua maranyingi uwezavyo

Muweke mtoto vizuri kwenye nyonyo ili kuongeza uzalishaji wa maziwa na pia kupunguza uwezekano wa kuumiza chuchu

Kutumia viungo mbalimbali katika vyakula vyako mfano, pilpili manga, mdalasini, hiliki nk.

Jaribu kuepuka msongo wa mawazo unaoepukika au tafutia suluhu msongo wa mawazo na sonona zitakazo jitokeza baada ya kujifungua.

Mfano wa vichupa vya kuhifadhia maziwa

Dalili zinazoonyesha mtoto anashiba vizuri

Mtoto ananyonya maziwa ya mama mara 6 mpaka nane kwa siku

Mtoto anapata choo kidogo zaidi ya mara 6

Wakati wa kunyonya unakuwa wa amani na furaha

Maziwa yanaisha kwenye nyonyo

Unaweza kumsikia mtoto akimeza mafundo ya maziwa

Mtoto anaongezeka uzito

Mtoto aendelee kunyonya maziwa ya mama mpaka umri wa miaka 2. Baada ya miezi 6 ya kwanza mtoto huanza kula chakula cha nyongeza mfano uji nk. Kutokana na sababu mbalimbali mama akashindwa kumnyonyesha mtoto wake anaweza kumpatia maziwa maalumu kwa watoto (infant formula). Kama familia inauwezo wa kifedha mtoto aendelee kutumia maziwa maalumu ya watoto na si ya ng‘ombe mpaka atakapo timiza umri wa mwaka mmoja.

3 COMMENTS

LEAVE A REPLY