Lini Unaweza Kumtoa Mtoto Wako Mchanga Nje.

0
3387

Lini unaweza kumtoa mtoto wako mchanga nje?

Wazazi wengi huofia kuwatoa watoto wachanga nje ya nyumba na kuwaweka ndani tu.

Kuna tamaduni zingine mama akishajifungua anatakiwa kukaa ndani na mtoto wake ndani ya nyumba mwezi mzima bila kutoka nje. Lakini hamna utafiti wa kisayansi ambao unasema sio vizuri kumtoa mtoto nje.

Hewa nzuri na mandhari nzuri na kubadilisha mazingira ni hali ambayo kila mtu anapenda na hii  hata  kwa watoto wachanga. Watu wengine wanasema ukimpeleka nje anaweza kupata magonjwa.

Jinsi ya kuepuka hili na kumlinda mtoto wako asipatwe na magonjwa akiwa nje basi jaribu kuweka kikomo wa muda ambao unataka akae nje na uwe nae karibu.

Kama kuna mtu anataka kumbeba pale wakati mmekaa nje kwenye mkeka hakikisha basi mikono yake ni misafi na wakati mwingine anawe kabisa maana kama mikono yake sio misafi anaweza kuleta magonjwa. Pia kama kuna mtu anaumwa basi muweke mtoto wako mbali nao asije kuambukizwa.

Yaani kama umemaliza kumlisha na kubadillisha nepi na yuko safi basi unaweza kumtoa nje akapunga upepo, hapa atakua tayari na fresh kulala kwenye hicho kiupepo kizuri wakati wewe upo pempeni unaendelea na shughuli zako.

Mvalishe mtoto wako nguo nzuri kama unapanga kukaa nae nje. Mvalishe nguo kulingana na hali ya hewa na umvalishe nguo katika hali ya kawaida kama vile ingekua ni wewe unataka kukaa nje. Sio unamvalisha sweta saa nane mchana alafu unamlaza nje, ingekua wewe ungevaa sweta mda huo na kukaa nje? Pia hakikisha unamuangalia jua maana kama ulimuweka kweye kivuli mida ya saa sita jua likisogea utakuta yupo juani kama hujamuangalia.


img_20161202_172004

LEAVE A REPLY