Kwa nini watoto hucheua mara kwa mara?

0
6493

Kwa nini watoto wanacheua kila mara?

Yaani hii kwanza ni ishara kwamba ameshiba. Ujue watoto wengi huwa wana hii tabia ya kucheua kwa hiyo usidhanie ni mtoto wako tuu, na muda ambao watoto huwa wanacheua sana ni wakiwa umri wa miezi minne.
Watoto wengine huwa wanakula kidogo na kulingana na size yao na kuna wengine wao wanapenda tu kula sasa katika hali hii unakuta mtoto anakua ameshiba sana mpaka anafikia hatua ya kucheua.
Mfumo mzima wa mmeng’enyo wa chakula wa mtoto unakua bado hauko sawa katika swala la kumengenya chakula vizuri.Mishipa ambayo inaweza kuzuia chakula kisitoke tumboni inakua bado haijakomaa kwa hiyo kucheua kunatokea tu bila hata ya wewe kujua.

Mambo gani ambayo unaweza kuyafanya?
Jaribu kufanya haya mambo alafu uone itakuwaje.
jaribu kumbeba mtoto wako vizuri na wima wakati unamlisha awe amekaa kwenye kiti au umembeba. Mkumbatie vizuri wakati anakula sio unamlisha huku amelala kwenye mkeka au kitandani, maana kuna watu wengine wanaamua kuweka khaga nyingine wanalaza chini ndio wanamlisha sio kwa hivo.
Panga ratiba ya kumlisha vizuri.

Kwanza wakati unamlisha ni vizuri kusiwe na kelele na vilevile usiwe na mambo mengine ya kukuchanganya yaani kama ukiamua kumlisha kaa chini tulia umlishe.
Jaribu kumlisha mapema kabla hajashikwa na njaa sana, inabidi uwe katika mazingira tulivu ili usimchanganye na kumsumbua sumbua maana ukimsumbua anameza hewa nyingi tumboni na matokeo yake ataanza kucheua hata kabla hujamaliza kumlisha.
Tumia Chupa InayofaaScreen Shot 2016-08-29 at 12.57.41 PM
Kama mtoto wako ameanza kunywa maziwa ya kwenye chupa basi hakikisha chupa ambayo anaitumia kitundu chake kisiwe kidogo sana vile vile kisiwe kikubwa sana. Tundu la chupa likiwa dogo linamsumbua mtoto kuvuta maziwa na uwezekano wa kuvuta hewa ni mkubwa, vilevile kama tundu la chupa ni kubwa maziwa yatakua yanakuja kwa spidi so utakua anavuta maziwa mengi kwa wakati mmoja.

LEAVE A REPLY