Dondoo za kumsaidia mama anaenyonyesha kuongeza uzalishaji wa maziwa

0
15554

Jinsi ya kuongeza uwezo wa kuwa na maziwa ya kunyonyesha

Kula Chakula Chenye Afya.
Yaani hiki ndio kitu cha kwanza kabisa kufanya kabla ya yote. Kama chakula unachokula hakina virutubisho vizuri mwilini mwako basi itakua vigumu kutoa maziwa ya kutosha mwilini kwa sababu katika hali ya kawaida wewe kama mama unatakiwa kula chakula kizuri ili mtoto wako naye apate chakula kizuri. Kwa hiyo mpangilio wa chakula unachokula inabidi uungalie vizuri, na vyakula unavyotakiwa kula ni vile vile tu vya kila siku, mboga za majani, viazi, vyakula vya asili na usipikie na mafuta mengi chemsha vizuri tuu, kunywa supu, matunda ya kutosha, yani ukila vyakula vizuri we mwenyewe hutokuwa na stress yoyote.

Mnyonyeshe mnyonyeshe mnyonyeshe.
Kama ulikua hujui ni kwamba kadri unavyomnyonyesha mtoto wako ndio uwezo wako wa kutoa maziwa mwilini unaongezeka. Usifate utaratibu wa kwamba kila saa ngapi sijui ndio unamnyonyesha noo, Mnyonyeshe mtoto wako kila mara anapojisikia ana njaa, usimpangie masaa ya kumnyonyesha ili mradi tu awe anataka kunyonya hasa kwenye week za mwanzo za kuanza kumnyonyesha baada ya kujifungua.

Usijali Tulia.
Yaani tulia kabisa wala usijali. Wakina mama wengi huwa wanafikiri kwamba wao hawana uwezo mkubwa wa kutoa maziwa kwa ajili ya mtoto na wakati hawana tatizo lolote. Ili mradi tu mtoto wako yuko vizuri, mchangamfu, na kila saa unambadilisha nepi basi ujue uwezo wako wa kutoa maziwa upo vizuri. Kumbuka inaweza kuchukua siku chache baada ya kujifungua maziwa kuanza kutoka so inabidi utulie tu.

Jaribu Kupumzika
Ukosefu wa kulala na kupumzika ni moja ya mambo ambayo yanaweza kukupunguzia speed ya utoaji maziwa. Kama unaweza kuchukua likizo ya muda kazini basi chukua maana ukichanganya kazi hiyo alafu urudi jioni umnyonyeshe na upo hoi inakua sio vizuri. Inabidi utenge muda wa kuwa na mtoto wako na ufanye kazi kidogo za nyumbani ili uwe na muda mwingi wa kupumzika, kula vizuri na kumnyonyesha. Sasa hii inawezekana kama ni mtoto wako wa kwanza, ila sasa kama kuna wengine ambao nao wanahitaji uwahudumie basi hapo ndio itabidi utafute msaada.

Punguza Stress
Wakati stress nayo inaweza kukupunguzia uwezo wa kutoa maziwa, na wakati mwingine stress inaweza kukufanya usipate hata hamu ya kumnyosha mtoto kwa wakati na hii itamsababishia mtoto wako asipate maziwa ya kutosha. Jaribu kujilinda na kuhakikisha hamna vitu vinavyokupa stress mara kwa mara. Muulize mwenzi wako, rafiki yako au ndugu yako akusaidie kazi zingine ili upate muda mzuri wa kuwa na mtoto, kama kuna wageni wakitaka kuja waambie watulie kwanza maana wakija hapo ndio utakua busy kuwahudumia kuhakikisha kila kitu kipo sawa na hapo sasa muda wa kuwa na mtoto utapungua.

Pata msaada.
Jaribu kutafuta wakina mama wengine ambao nao wananyonyesha na ujifunze kutoka kwao. Kama mama yako au rafiki yako au hata bibi yako naye alinyoshesha muulize ilikuaje na utapata mambo mengi hata mama yako muulize wakati anakunyonyesha ilikuaje utajifunza vitu vingi. Kama unajiona uwezo wako wa kutoa maziwa ni mdogo na haukupi furaha basi jaribu kujiepusha na watu ambao hawana msaada kwako au wanakupa wakati mgumu wakati wa kunyonyesha.

Acha kunywa bia na kilevi chochote.
So unaweza kusikia au kama ulikua hujawahi kusikia eti wanasema ukinywa bia huwa inasaidia kuongeza uwezo wa kupata maziwa mwilini duh!!!,….jamani ukweli ni kwamba bia ndio inapunguza uwezo wa kuwa na maziwa mwilini.

ts_150317_breast_feeding_baby_800x600
Hii ni kitu ya kawaida kabisa. Inabidi kila mara ujikumbushe kunywa maji kila mara maana kama mwili hauna maji mwilini uwezo wa kutoa maziwa utakua ni mdogo. Ni rahisi sana kubanwa na kazi zingine za kumhudumia mtoto na nyumba kwa hiyo kaa na chupa ya maji pembeni ili uwe unakunywa kidogo kidogo. Pia jaribu kula matunda ambayo ya maji maji matunda, mboga mboga za majani.

LEAVE A REPLY