Jinsi ya Kudeal na Watoto Wakati wa Chakula

0
3917

     55bd3b9744a696559292bc34662a965b8db7de61Jinsi Ya Kudeal na Watoto wakati wa Chakula

Wote tunajua jinsi gani watoto huwa wanapenda kuchagua vyakula eh? Kwanza wanataka kula chakula cha aina moja tu wanachokipenda, ukimpa chakula kingine ni ugomvi mpaka kero, na wanapenda kweli kula vyakula ambavyo havileti afya, yaaaani wanataka chips , pipi, soda, crips, ila sasa mpe uji……. Nahisi                                                                   unajua nini huwa kinatokea.

Huwa inakua ni ugomvi kwa mzazi ukifika wakati wa kumpa mtoto chakula, kwa wototo ambao bado ni wadogo pre-school wao huwa ni kawaida kuchagua chagua chakula ila baaadae wanavyokua huwa wanabadilika. Muda wako wa kula unaweza kuathiri mtoto wako, kama mzazi ni kazi yako kumpatia mtoto wako chakula chenye afya, sio lazima chakula kiwe cha gharama, vyakula vya kawaida tu. Wazazi mnatakiwa kupanga mda wa kula chakula cha kawaida na muda wa kula snacks. Ukimpa snacks mtoto wakati ni muda wa kula chakula hapo kesho ukija kumpa chakula kingine mnaweza kuzua ugomvi. Mpangilio wakati mwingine unaweza usiende sawa kutokana na kazi za wazazi wenyewe ila tafadhali jaribu kuhakikisha ratiba yenu ni ya kila siku. Yaani usimlishe leo saa saba, kesho ukamlisha saa tano mara keshokutwa saa nane hivyo unakua unamchanganya kabisa, Hivyo kutokana na ugumu wa kazi zako angalau jaribu kupangilia muda mmoja wa kumpa chakula.

Mwenendo mzuri wa lishe bora kwa mtoto

Kama mtoto wako anaendelea kukua vizuri pamoja na katabia chake cha kuchagua chagua vyakula basi tambua kuwa vyakula unavyompa ndio vinamfaa. Endelea kumpa hivyo hivyo vyakula, kama ni uji, ndizi zilizopondwa, wali kama anakula, mkate mpe apate afya hata samaki. Ila sasa kama upo na mtoto ambaye amekataa kuacha kuchagua vyakula basi kuna baadhi ya vitu unatakiwa kufanya illi kumfanya na yeye avipende hivyo vyakula.

Kwa mfano.

 • Pika chakula chenye afya na uweke kwenye sahani yako na yeye muwekee mle kwa pamoja.
 • Mkaribishe mtoto wako mpange mnapika chakula gani; Hii itamfanya na yeye ajisikie wakipekee na kama vile ameandaa chakula kwa hiyo kikiiva ni matumaini kwamba atakula hicho chakula.
 • Kula chakula kwa pamoja na familia mezani; Usimpe chakula peke yake alafu badae  wewe na watu wengine wa ndani mnakula, kuleni nae kwa pamoja, ni muda mzuri wa kuongea na kumfundisha kula vyakula vyote kama akiwaona wote mnakula hicho chakula. Hii inasaidia sana kwa sababu mtoto hatakua na muda wa kuanza kuchambua hicho chakula kwa sababu anaona wote mnakula.
 • Upishi Mzuri; Hamna kitu ambacho huwa kinaumiza kama kula chakula ambacho hakijapikwa vizuri. Kwa hiyo hapa unahitaji upike chakula vizuri kiive, na kama kuna manjonjo unataka kuongeza yaweke ili chakula kiwe kinavutia kwa mtoto akipende. Sasa kama utapika chakula kwa juu juu usishangae mtoto wako akiwa anakataa chakula.
 • Muulize mtoto anataka nini; Hii ni njia nyingine ya kumfanya mtoto ajisikie special. Akichagua chakula cha ajabu ajabu mwambie utampikia jioni ila mchana atakula ndizi au mchicha. Maana kuna watoto wengine mboga za majani hawapatani nazo.
 • Mfanye mtoto wako awe mchangamfu. Mtoto akiwa mchangamfu anacheza cheza cheza sana kama kawaida lazima atakua na njaa na hapo sasa hata ukimuwekea viazi vitamu lazima atakula tu mpaka ashibe. Ila sasa ili asinune sana unampa na juice anayoipenda hapo mtaendana sawa.

Kumbuka……..kuwa mpole na mvumilivu. Kujaribu vyakula tofauti huwa inachukua mda. Usishangae kama utajikuta unajaribu kumpa mtoto wako vyakula tofauti tofauti mara ishirini ndio unaona anaanza kuvipenda.

Vitu vya kuzingatia.

Usidhanie kuwa kama mtoto wako anachagua chagua vyakula basi ukipika chakula ambacho unajua hakipendi itakua ni ugomvi. Ukifanya hivyo mtoto atagundua kuwa umekasirika na hapo ndio utakua umeongeza tatizo jingine kabisaaa. Kuwa mpole na mvumilivu usimuonyeshe kama umekasirika. Ngoja nikwambie vitu vya kuboresha

 • Usimuwekee chakula kingi. Hii iko hivi kama mtoto hapendi mboga za majani kama ukimuwekea mboga za majani nyingi kwenye sahani hapo ndio hutawezana nae, sasa cha kufanya chukua sahani kubwa muwekee mboga kidogo tu, hapo ataona sahani ni kubwa ila chakula ni kidogo kwa hiyo hatoona ni tabu kula hicho chakula kuliko ungekua umemjazia sahani nzima.
 • Usimlazimishe kula. OK hapa ndio huwa kuna balaa. Watoto wetu hawa wa siku hizi bila kumlazimisha kula haendi. Ila unashauriwa usimlazimishe kula kwa nguvu kwa mda mrefu ukifanya hivyo inakua ni ugomvi……mpeleke taratibu tuu.
 • Usipike chakula cha kipekee kwa  kila mtu wa ndani. Pika chakula kimoja ambacho wote mnakula sio kila mtu na chakula cha aina yake. Mara huyu anakula viazi, mwingine amakula wali.
 • Usiwe na hofu kama mtoto wako hali vyakula vyenye afya kwa sana maana mtoto wako ndie anayeamua ni kiasi gani cha chakula anataka kula, cha muhimu uhakikishe anakula hivyo vyakula haijalishi ni kwa ujazo gani.
 • Kama muda wa kula unaona ni ngumu basi subiri atulie kisha umbembeleze taratibu huku ukimlisha,hakika atakula.

Na,

Irene K Kiwia

 

 

 

 

 

SHARE
Previous articleNIDHAMU
Next articleUFAHAMU UGONJWA WA PUMU (ASTHMA)
Irene Kiwia
Irene Kiwia ana shahada ya Uhasibu 2015 na pia anatarajia kuanza shahada ya uzamili 2016/17. Tofauti na kua na taaluma na uhasibu, anapenda sana uandishi na usomaji vitabu. Alivutiwa na kuandika articles mbalimbali katika toleo la kwanza mtoto magazine kwa sababu alikuwa ni mama mtarajiwa na alipenda kua mama bora na kuelimisha wengine kuhusu malezi ya mtoto kwa sababu aliamini hakuna njia ya kua mama mkamilifu lakini kuna njia zaidi ya elfu moja ya kua mama mzuri kwa mtoto wako.

LEAVE A REPLY