UNAMFAHAMU WORLD’S YOUNGEST MOTHER??SOMA HAPA KAMA HUMJUI!!

0
1216

Umeshasikia mtoto kapata mtoto,huyu ndio anashikilia record ya dunia kwa kuzaa akiwa na umri mdogo.

Lina Medina mtoto wa miaka mitano (5)….wa Ticrapo nchini Peru mwaka 1939 alizaa mtoto wa kiume na akaitwa Gerardo.Wazazi wake walidhani ana uvimbe tumboni alipopelekwa hospitali kupimwa akakutwa na ujauzito wa miezi saba.
Lina alikuwa mtoto wa kawaida kama watoto wengine tu lakini kwa mujibu wa baba yake alishaanza kupata periods zake mapema.Jina la mtoto wake Gerardo lilitokana na jina la daktari aliyemuhudumia.

PhotoGrid_1497250774903
Ishu ya Lina iliwasumbua sana madaktari imewezekanaje yeye kupata mtoto?baba wa mtoto?alibakwa?
Baba wa Lina alifunguliwa mashtaka ya kuhusishwa kumbaka lakini alikuja kuachiwa baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha.Lina mwenyewe hakuwahi kusema alipataje huo ujauzito.Baba wa mtoto wa Lina hakuwahi kujulikana na hata namna ambavyo mtoto huyo wa miaka mitano alivyoweza kupata ujauzito.
Kwa sababu ni jambo lisilo la kawaida madaktari walijaribu kufanya tafiti za kila aina.Baada ya research iligundulika Lina alikuwa na tatizo la hormone disorder na madaktari walitaka akae hospital kwa uchunguzi zaidi wa kisayansi lakini familia yake ilikataa.Wakamchukua mtoto wao na kumlea yeye na mtoto wake pamoja na mdogo wake.Mtoto wa Lina alilelewa kama mdogo wake na hata akikuwa alijua Lina ni dada yake mpaka alipotimiza miaka 10 ndio alijua kuwa ni mama yake..
wenye maisha yake ya usichana alifanya kazi ya usecretary kwenye Lima clinic.Hii ni clinic ya Dr. Lozada aliyejitolea kumsomesha yeye na pia kumsommesha mtoto wake high school.

PhotoGrid_1497250806651

Alikuja kuolewa na kupata mtoto wake mwingine mwaka 1972 akiwa na miaka 39.Mwaka 2002 waandishi wengi wa habari walimfata kwa mahojiano wakiwemo Reuters lakini aliwatolea nje kuongelea chochote kuhusu maisha yake.
Mwaka 1979 mtoto wa Lina Gerardo alifariki dunia akiwa na miaka 40 kwa matatizo ya bone marrow.
Na inasemekana Lina Medina bado yu hai akiwa na umri wa miaka 83 hivi sasa.

LEAVE A REPLY