VIASHIRIA KWAMBA UNATAKIWA KUACHA KUFANYA MAZOEZI NA KUMUONA DAKTARI WAKO.

0
1883

Habari yako ndugu msomaji,naamini upo salama kabisa na umepata nafasi nyingine njema yakujifunza na mimi. Tumekua na mjadala mfululizo wa swala zima la mazoezi kwa mama mjamzito na leo nataka tuone kwa kifupi kabisa viashiria ambavyo ukiviona kama mama kijacho inabidi uache mazoezi nakumuona daktari na kumuelezea viashiria hivyo.

  • Maumivu makali ya kicha wakati au baada yakufanya mazoezi.
  • Kusikia kizunguzungu na muda mwingine kuhisi hali ya kupoteza fahamu wakati wa mazoezi au baada.
  • Maumivu kwenye kifua wakati na baada ya mazoezi.
  • Kupata aina yeyote ya uvimbe,au kwa lugha nyepesi kuvimba,kama miguu au sehemu yeyote wakati wa mazoezi au baada. Muone daktari.
  • Kupata shida ya kutembea na maumivu makali,muone daktari wako na acha mazoezi mara moja.
  • Kutokwa na damu ukeni.
  • Mabadiliko ya mzunguko wa mwanao au kutosikia mzunguko wake kwa namna ya kawaida.
  • Udhaifu wa misuli muone pia daktari na acha mazoezi maramoja mpaka utakapo pewa muongozo mzuri wa kufanya mazoezi au muongozo wowote utakao kua afya kwako na kwa mwanao.

kumbuka kwa mama yeyote furaha yake ni kuona mtoto wake anakua salama,na usalama huo unaanza kuujenga toka akiwa tumboni. Wataalamu wanasema mtoto anasikia na kuna namna anahisi upendo wa wanaomzunguka na walio karibu yake kwa nje hususani mama yake na baba yake kama watakua na ukaribu naye. Hivyo muonyeshe upendo huo kwa kuakikisha unakua salama kwa ajili yake na afya yake kiujumla,na ndo maana muandishi nashauri ukiona hayo maumivu hapo juu kabla au hata baada ya mazoezi muone daktari na uache mazoezi mara moja mpaka utakapo pewa muongozo wa kitaalamu.

Mpaka wakati mwingine tena,endelea kujifunza zaidi.

LEAVE A REPLY