USAFI WA MAMA ANAENYONYESHA

0
2422

Kipindi unanyonyesha kuna usafi unahitajika lakini usafi huo pia unatakiwa uwe wa kiafya  ili kumlinda mtoto na maambukizi ya bacteria na mambo mengine. Usafi huo ni wa kipekee tofauti sana na maziwa ambayo sio hanyonyeshwi. Zingatia mambo yafuatayo kuhakikisha usafi wa maziwa kwaajili ya afya yako na mtoto pia;

  • Usioshe maziwa au matiti yako kwa kutumia sabuni ya aina yoyote.
  • Usipake mafuta yoyote kwenye maziwa (matiti) yako.
  • Usipulizie malashi au manukato ya aina yoyote kwenye maziwa au karibu na maziwa au chuchu zako.
  • Usirudie nguo hasa sindilia au brazia.
  • Oga mara kwa mara kuzuia harufu mbaya.
  • Osha maziwa yako kabla ya kumnyonyesha mtoto na baada ya kumnyonyesha na ujiweke katika hali ya usafi.

Kwanini tuzingatie hayo yote? ukiosha maziwa yako kwa sabuni unamlisha mtoto makemikali ya sabuni hiyo sio afya utamsababishia magonjwa, vivyo hivyo kwa kwenye mafuta na malashi anaweza kupata chafwa na kupata shida ya kupumua kwa sababu ya harufu ya manukato hayo hivyo huna budi kujizuia kufanya hivyo kwaajilia ya afya ya mtoto. Usirudie nguo hasa sindilia kwa sababu italeta harufu mbaya ya jasho na mtoto anaweza kupata bakteria kupitia uchafu huo. Kuondokana na harufu mbaya hizo jitaidi kuoga mara kwa mara kwa maji safi na salama na kuvaa nguo safi kwa afya bora ya mtoto na wewe.

 

LEAVE A REPLY