ANGALIA MANENO YA KUONGEA UKIWA MJAMZITO!!

0
9221

Wanawake wengi hudhani malezi ya mtoto huanza akishazaliwa na wengine huenda mbali zaidi na kuhisi mtoto analelewa na kufundishwa akifika umri fulani, hayo mawazo yote  yanaukweli ila sio sahihi. Malezi ya mtoto huanza pale tu mimba inapotungwa na hivyo yakupasa kujua namna ya kulea kitu usichokiona, na ujue tu mna mawasiliano ya moja kwa moja hivyo tambua nini cha kuongea;

  • Epuka lugha chafu kama za matusi, kejeli na masengenyo
  • Epuka maneno ya kujutia mimba yako na manung’uniko
  • Epuka maneno ya lawama na ya hasira.

Kwanini uepuke hayo? kisaikolojia unamuathiri yule mtoto tumboni kwa sababu hali ya mama inamtengeneza mtoto moja kwa moja. Hivyo ni hekima na busara kujiepusha na maneno na matendo mabaya kwa faida ya mtoto mwenye afya. Itafute amani na moyo wako uwe wenye afya kwa sababu yako na huyo uliembeba. Jiongelee maneno mazuri, mwambie mtoto wako unampenda akiwa bado tumboni, epuka stress.

LEAVE A REPLY