VITU HATARISHI VIWEKWE MBALI NA WATOTO

0
1363

Watoto tofauti na watu wazima wanatabia ya kutaka kujua kila kitu na kwa umri fulani wanapenda kula kila wanachokiona bila kujali mazingira waliopata kitu icho. Ni hatari sana kipindi icho wazazi na walezi unabidi wawe makini kuliko kawaida,epuka vitu vifuatavyo;

  • Kuweka dawa za wadudu,mimea,wanyama karibu na mazingira ya watoto. Kwa mfano dawa ya panya.
  • Vidonge vya aina yoyote
  • Vipodozi
  • Na vitu vyote hatarishi kwa afya ya mtoto

Kuna dawa za wanyama kama Panya ambazo hua kama tambi huweza kuwavutia watoto na tusipokua makini watoto wanaweza okota na kuvila na kuleta madhara makubwa kwao. Vivyo hivyo kwa dawa zingine za kupuliza na vidonge ni hatari hivyo vinapaswa kuwekwa mbali na watoto. Kwaajili ya kuepuka majanga mbalimbali kwa watoto wetu hatuna budi kuwalinda na kuwa makini na njia zote wanazopitia katika ukuaji wao.

LEAVE A REPLY