JINSI YA KUZUIA MTOTO KUKOJOA KITANDANI

0
4227

Mtoto kukojoa kitandani inazuilika na mara nyingine sio hata ugonjwa ni malezi tu. Ingawa mara nyingine hua ni ugonjwa na huitaji ushauri wa daktari na hutibika kabisa. Hapa tutaangalia njia za kuzuia mtoto kukojoa kitandani kwa wale ambao hawana matatizo ya kitabibu;

  • Njia ya kwanza ni kuthibiti unywaji wa vimiminika masaa machache kabla ya kulala au wakati wa usiku.
  • Hakikisha anaenda kukojoa kabla hajaenda kulala na ulisimamie hili.
  • Njia ya pili ni kumuamsha wakati wa siku kwaajili ya haja ndogo ili kuzuia kukujoa kitandani, mara kwa mara. Weka ata alamu ikukumbushe kila baada ya masaa mawili au matatu. Kesho yake akikojoa tena rudisha yale masaa na umwamshe baada ya lisaa limoja na nusu kila siku.
  • Njia nyingine ni Asali mbichi, mpe mtoto kijiko kidogo cha asali mbichi kabla ya kulala kila siku, mpaka atakapo pona. Unaweza kumpakia kwenye mkate wakati wa chai asubui.
  • Mdalasini pia ni dawa nzuri sana kwa watoto wenye matatizo ya kukojoa kitandani, huufanya mwili wa mtoto kupata joto ambalo huzuia kukojoa kitandani. Chukua unga wa mdalasini kijiko kidogo kisha changanya na asali halafu paka kwenye mkate au ukachanganya kwenye maziwa fresh.
  • Masaji, hii pia ni dawa nzuri kwa kuzuia kukojoa kitandani, tumia mafuta ya zeituni (olive oil) yachemshe kidogo yapate uvuvugu alafu mmasaji mtoto chini ya tumbo. Fanya ivo mara kadha, masaji taratibu taratibu.

Usimpige mtoto kwa sababu ya kukojoa kitandani wala kumfokea bali mlee kwa upendo na uwe unampa zawadi kila mara asipokojoa kumpa moyo. Pia usiku uhakikishe njia ya kwenda chooni inamwanga wa kutosha kwa kua watoto huogopa giza pamoja na hilo msindikize mpaka atakapokua na uwezo wa kwenda mwenyewe. Fanya mambo kwa upendo nae atakua anaelewa na kuacha kukojoa kitandani. Kama izo njia zote zikishindikana mpeleke kwenye kituo cha afya kwa utatibu zaidi.

LEAVE A REPLY