NJIA ZA KUZUIA KUTAPIKA WAKATI WA UJAUZITO

0
13504

Kutapika kwa mama mjamzito inaleta kero na mama huyo kukosa raha mara nyingi. Miezi ya awali ya ujauzito hua na changamoto hii sana lakini ikiendelea inaleta karaha kabisa, unaweza kuzuia hali hii kwa njia zifuatazo.

 • Kula matunda au mkate wa kukaushwa asubui
 • kunywa vinywaji nusu saa kabla ya kula au baada ya kula. Usile na kunywa kwa wakati mmoja.
 • Kunywa maji mengi sana kuzuia upungufu wa maji mwilini (dehydration). Jitaidi kunywa lita 2.5 kila siku na pamoja na juisi ya matunda.
 • Epuka kulala baada ya chakula
 • Pata muda wa kupumzika wa kutosha na pata kusinzia mchana
 • Fanya mazoezi
 • Ndimu na tangawizi husaidia kupunguza na kuondoa kichefuchefu. Unaweza kunywa juisi ya ndimu au tikiti maji.
 • Epuka kupita sehemu yenye harufu ya chakula
 • Epuka kula vyakula vyenye pilipili au viungo vingi
 • Pata hewa (Oxygen) ya kutosha na fungua madirisha ili hewa iweze kuingia
 • Usiache kula au kuruka milo.

Hizo ni kati ya njia chache za asili kati ya nyingi. Tatizo likizidi muone daktari kwa matibabu zaidi na vipimo zaidi

LEAVE A REPLY