KUMPA MTOTO HELA…VITU GANI UNATAKIWA KUJUA

0
1519

KUMPA MTOTO HELA. VITU GANI UNATAKIWA KUJUA

Kwanza Kwanini Umpe Mtoto Hela?

Ili mtu ujue kuendesha baiskeli unahitaji uwe na baiskeli. je ukitaka kujifunza thamani ya Pesa na matumizi unahitaji nini? Pesa. kwa kumpa mtoto hela ni njia moja wapo ili ajifunze jinsi ya kutumia hela na thamani yake na kujifunza pia jinsi ya kuweka akiba na kupangilia matumizi yake kwa ujumla, na kwa hiyo unakuta unatakiwa kumpa hela kidogo ili aanze kujifunza mapema hivyo vitu huku unamfatilia.

Ukimpa mtoto hela unamruhusu kufanya makosa ambayo hayana madhara makubwa na kwa kuwa bado yuko chini yako unamuelekeza. Ni kama kumfundisha mtu kuendesha gari kwenye uwanja wa mpira asubuhi ambapo hamna mtu hata mmoja uwanjani. Kama umeshawahi kuwaona watu wanojifunzia kuendesha uwanjani we unafikiri ni kwanini hawaanzii barabarani moja kwa moja.

Kama mtoto wako hawezi kufanya kitu flan kwa sababu hela uliyompa alitumia kwenye mambo mengine, next week atajifunza jinsi ya kupangilia matumizi yake, na wakati unamfatilia mfundishe kabisa kuwa kuna baadhi ya vitu anatakiwa apangilie mwenyewe na ajinunulie kutokana na hela uliiyompa.

Umri Gani Mzuri wa Kuanza Kumpa Mtoto Hela?

Kuanzia umri wa miaka 6 au 7. Ila kuna wazazi wengine tangu katoto kana miaka mitatu tayari ameshaanza anza kukashikisha hela, na wengine mtoto akishaanza tu kwenda shule tayari na yeye anaanza kumpa hela na wengine wanasubiri kabisa mpaka afikishe miaka kumi ndio anaanza kumpa hela, kwa hiyo unakuta kila mzazi ana style yake ya kumlea mtoto wake. Yaani muda mzuri ni pale ambapo mtoto wako atakua ameshagundua kuwa hela inaweza kumfanya akanunua kitu anachokitaka. Mtoto wako akishagundua kuwa akitaka kalmu lazima inunuliwe, au pipi lazima inunuliwe na sio ya kuokota basi huyo atakua ameshaelewa hela ni nini.

Shingapi Unaakiwa Kumpa na Mara Ngapi?

Hii kwanza ni wewe mwenyewe kuamua ni kiasi gani unaweza kumpa kulingana na kipato chako ukijumlisha matumizi ya nyumbani na matumizi ambayo mtoto wako anaweza kuwa nayo, kwa hiyo unakuta ni wewe mwenyewe kuamua ni kiasi gani unaweza kumpa.

Ila kwa kukusaidia tu unaweza kutumia njia umri. Mfano Kama ana miaka 5 unampa 5000/= au 2500 kwa week akifikisha miaka sita unaongeza 6000/= au 3000/= kulingana na miaka yake. Hii njia inafaida kwa sababu kama unawatoto wawili mdogo ataelewa kwa nini dada yake anapata 1000/= aalafu yeye anapata mia 500/= ni kwa sababu tu dada yake anamzidi miaka kwa hiyo haina ubishi.

Jinsi ya Kufundisha Mtoto Wako Kuweka Akiba.

Hapa sasa ndio muda mzuri wa kumfundisha mtoto wako kuweka akiba. Njia nzuri ni wakati unaanza mpe hizo hela kama miezi mitatu ya mwanzo wala usimwambie kuhusu swala la kuweka akiba. Alafu baada ya hapo uje uongee nae na kumuuliza kama kuna hela ya akiba aliyoweka sehemu ndani ya hiyo miezi mitatu. Mara nyingi utakuta wala ahajaweka. So Ukikuta hana hapo hapo unampa somo na kumwagiza kila mwezi aweke akiba anayoiweza yeye mwenyewe. Usimpangie shilingi ngapi aweke, we mwambie tu kila mwezi unataka kuona ameweka akiba yoyote.

LEAVE A REPLY