Njia Rahisi za Kufundisha Mtoto Wako Thamani ya Pesa

0
1371

 

Njia Rahisi za Kufundisha Mtoto Wako Thamani ya Pesa.

Watoto wakishapata uelewa huwa unaweza kuanza kuwafundisha jinsi ya kutumia pesa na kuijua thamani ya pesa. Ila sasa tutawafundishaje hawa watoto jinsi ya kuthamini hizo pesa, maana siku hizi mtoto hata hajafikisha umri wa kushika pesa tayari kaishajua shilingi mia inavyofanana.

Nenda Nae Bank.

Kwenda na mtoto bank ni njia nzuri sana ya kumfundisha kuhusu mambo ya pesa kuliko kumletea pipi nyumbani jioni. Hata mtoto mdogo wa miaka minne anaweza kumpa mtu wa bank karatasi ya kutolea hela uliyojaza. Mpe akampe pale dirishani aone mwenyewe hela zinapotoka na aone watu walivyopanga foleni mpaka nje ya mlango. Baada ya hapo unamwambia nini kinaendelea hapo na hapo ataelewa.

Mtoto wako kadri anavyokua mfungulie na yeye account yake ili aanze kuisimamia mwenyewe na umsimamie jinsi anavyo tunza hela zake na matumizi yake kwa ujumla.

Mwambie Akusaidie Kulipia Bili Mbalimbali Anazoweza.

Mtoto wako akishaanza kuweza kusoma na kuandika mwambie awe anakusaidia kulipia bili mbali mbali za nyumbani au mpe kazi tu ya ziada ya kufatilia matumizi ya nyumbani na awe anakukumbusha kabla hayajaisha, iwe ni umeme, maji, gas, hata mafuta ya gari, au hata hela ya mwenye nyumba (Kodi) mwambie viko chini yake na ahakikishe kabla havijaisha akwambie.

Hiyo inamjengea yeye uwezo wa kujua matumizi ya nyumbani yakoje. Maana unakuta mtoto mkubwa wa miaka hata 12 au 17 hajui kwa mwezi ndani wanatumia umeme wa shilingi ngapi au gas inanunuliwa mara ngapi ndani ya mwezi.

Mpitishe Mashambani.

Watu tunavyoenda kununua vitu sokoni au super market huwa tunapenda kwenda na watoto ila kule mtoto hajui hizo carrot na nyanya zimetoka wapi. So siku weekend zako umeamua kwenda shamba nenda nae akaone sehemu zinapotoka na kama ni kununua mwambie akusaidie kuchagua na umpe hela alipe yeye mwenyewe na achukue chenji. Hiyo ni njia nzuri ya kumfundisha mtoto kwa vitendo kuliko kukaa nae sebule ni na kumwambia nyaya zinalimwa na wakulima na wakati hajawahi kukutana hata na mkulima mmoja. So wakati mwingine unapopanga safari unaweza kuwaza mwenyewe kama unaweza kwenda nae akajifunze kitu mchukue kazurure nae……tusiishie kwenda nao sokoni.

Mfundishe Jinsi ya Kuweka Akiba.

Mtoto wako bado ana vitu vingi vya kujifunza kuhusu pesa na njia nyingine ya kujifunza ni kumuelekeza jinsi ya kuweka akiba. Hii ni kitu rahisi we tafuta box la kuwekea akiba na uliweke zehemu ndani na kama familia muwe mnadunduliza humo baadhi ya chenji zinazorudi. Kisha unamuelekeza hiyo ni nini na hata yeye mkishaanza kumpa vijihela mumwambie na yeye awe anachangia. Maana kuna wakati hawa watoto nao huwa wanamahitaji ya ajabu ajabu halafu huwa ni bei ghali sasa njia nzuri ya kumfundisha ni kuwa na hilo box na kumwambia hilo box likifika nusu tunaenda kununua hicho kitu anachokitaka. Ila wewe ushajua hata kesho unaweza kumnunulia ila unamfundisha tu jinsi ya kuweka akiba kwa ajili ya kitu flani.

LEAVE A REPLY