Tips za Kulea Mtoto Wa Kike

0
2207

Tips za Kulea Mtoto Wa Kike

Watoto wa kike huwa wana speed ya hatari sana. Kwanza huwa wanaanza kuongea mapema utakuta anaongea sanaaa na kupiga kelele kila mara, mara anataka kugusa hiki na kile yaani ni balaa kila kona ya nyumba.

Basi zifuatazo ni tips ambazo unaweza kuzitumia wakati una mkuza huyu mtoto wa kike.

Mfundishe Kuwa Jasiri.

Mfudishe mtoto wako kuwa jasiri na kuonyesha hisia zake kwa mama au baba au hata shangazi yake, awe jasiri. Mwambie kabisa kama kuna mtu shuleni anamchezea chezea amwambie kabisa mbele yake kuwa hapendi hicho kitu sio kuogopa kumwambia.

Mpongeze vitu Vizuri Kwa Undani.

Kuna tofauti kati ya “Hongera” na “Hongera kwa kufaulu mtihani wako” watoto wa kike ukimpongeza kitu mpongeze kwa undani na utaje kitu alichokifanya ili ajue kabisa kuwa ametenda jambo jema. Usiishie tu kusema hongera au umependeza. Sema ” Umependeza na gauni lako nimelipenda kweli”

Muelezee Vitu Aelewe Vizuri.

Kama mtoto wako anakwambia tatizo lake la shuleni kuhusu marafiki au walimu, kaa nae chini kwa muda tuu au wakati unaendesha kwa undani kwa nini rafiki zake wamemfanyia hivyo au kwanini mwalimu kamfanyia hivyo ili aelewe vizuri. Maana wasichana walivyo hawachelewi kumnunia mwalimu mwezi mzima kwa sababu hajaelewa tuu kwanini mwalimu alifanya vile, so wewe ukimuelezea unatoa utata wake.

Mshawishi Afanye Kazi Zake Mwenyewe.

mtoto wako akirudi na homework zake hapo akakuuliza umsaidie, jamani usikimbilie na kuanza kumsaidia tuu, hii hata kwa wavulana. Mwambie kwanza yeye afanye alafu baadae utakuja kumsahihisha.

Usidhanie Kuwa Hawezi au Anaweza Kufanya Kitu Flani.

Kwa sababu ni mtoto wa kike unaanza kuwaza hawezi kucheza mpira wa miguu au hawezi kusoma sayansi. Haimaanishi kuwa hatotaka kufanya hivyo vitu kwa sababu tu ni mtoto wa kike, we muache na ufatilie muenendo yake na umsaidie sehemu ambayo atahitaji msaada.

Ongea Nae Kuhusu Mambo ya Urembo na Uzuri.

Siku umekaa tu hapo hujui hili wa lile anakuja hapo anakuuliza “mama eti mimi ni mzuri?” kwanza lazima utashangaa nini kimemkuta mpaka akauliza hilo swali….. ila hilo ni swala la baadae kwa sasa baada ya yeye kuuliza hilo swali Yaaani mjibu NDIO ya herufi kubwa tena kama kuna kioo acha unachokifanya mpeleke kwenye kioo umuonyeshe jinsi alivyo mzuri. Ukifanya hivyo yaani unamuondolea maswala ya kuwaza tena kuhusu maumbile yake na mambo ya urembo kwa sababu mama yake mwenyewe au baba yake mwenyewe anamkubali kuwa yeye ni mzuri na umwambie kabisa maneno ya watu kuwa eti yeye sio mzuri ni wivu tu. Yeah Mwambie hivyo kabisaaaa!!

Muandae Kuhusu Mambo ya Jinsia.

Mpaka hii leo kuna watu wanaamini kuwa kuna baadhi ya kazi wasichana hawawezi kufanya na zinafanywa na wavulana tu. Kwa hiyo inabidi mara kwa mara uwe unampa mafunzo ya kijinsia kuwa kila kazi anaweza kufanya na yeye ana nafasi sawa na watoto wa kiume na asiwe nyuma nyuma kwa sababu tu kuwa yeye ni wa kike, kama ushaelewa naongelea nini hapo eh. Muonyeshe kuwa hakuna maswala ya kike au kiume, wote ni sawa. Tena kama ndani ya nyumba kuna watoto wakiume na wa kike usitenge kazi za kiume na za kike wote wafanye kazi sawa mtoto wa kiume na yeye aoshe vyombo, kazi ya kuosha vyombo isiwe ni kazi ya neema tu au maria na john na yeye aoshe.

LEAVE A REPLY