Tips za Kulea Mtoto Wa Kiume.

0
2752

Tips za Kulea Mtoto Wa Kiume.

Ok so umetoka kujifungua na umepata mtoto wako mzuri wa kiume. Good for You! so kwa kifupi tu wala sitaki kuongea maneno mengi nataka nikupe tips mbili tatu ambazo unaweza kuzitumia wakati unamlea huyo little boy.

Mpe Majukumu.

Kufata maelekezo na kumaliza kazi wanazopewa wavulana hii kitu huwa ni changamoto sana kuizoea. kwa hiyo akiishaanza kukua mzoeshe kumpa vikazi vidogo vidogo ambavyo anaweza kufanya ili aanze kuzoea mapema kufanya kazi mbali mbali na kuzimaliza kama ulivyomuelekeza. Kama unapika mwambie akuletee ungo, au mwiko hivi vikazi nahisi utakua unavijua, ila kama ulikua hujui hivi vikazi vinasaidia sana mtoto kujifunza namna ya kufanya kazi, kwa hiyo usione kama unamsumbua maana wazazi wa siku hizi kwa upendo tunaongoza.

Muache Akuonyeshe Hisia Zake.

Hata kama ni nyakati za furaha wavulana huwa hawaonyeshi ile furaha mpaka mwisho huwa wanafanya kimya kimya kimoyo au mpaka awe peke yake, kuliko wasichana ambapo anaweza furahia na kuruka ruka hapo sebuleni mpaka jikoni bila shida. So mvulana wako mwambie aonyeshe hisia zake kama kakasirika muache aonyeshe kuwa amenuna ili mradi awe mstaarabu tu asiwe anavunja vitu. Baada ya kumaliza biashara yake ya kununa hapo sasa unaweza kurudi na kuongea nae akwambie nini kinamsibu kuliko kumkatisha masikitiko yake. Kwa maneno mengine wakati wa huzuni kama amekasirika muache akasirike mpaka amalize halafu ndio uje uongee nae.

Usijali Kama Haonyeshi Tabia za Kiume Wakati Mdogo.

Kama mtoto wako bado ni mdogo na bado anapenda kuchezea midoli muache aendelee, au ameshaanza kwenda shule na bado unamuona anachezea midoli au anapenda sana katuni, hiyo sio kwamba ni wa ajabu ila ndio umri wake wa kukua kwa hiyoo usidhanie bado ana matatizo flan.Mtafutie michezo zaidi ya watoto wa kiume vigari,baiskeli,mpira wa soka n.k

Msaidie Kutengeneza Marafiki na Mambo ya Kijamii.

Wavulana wengi mara nyingi huwa ni wagumu kutengeneza urafiki na mtu kuliko wasichana. wanaweza kucheza kwenye kikundi au group baada ya hapo yuko kivyake, kwa hiyo hapo anahitaji msaada wako ukiona hivyo kwa kumuunganisha na mtoto mwingine ili atengeneze urafiki wa karibu na watu mbalimbali na umwambie wacheze wote hata kutumia vigari vyake.

Mpe Support Kwenye Mambo Yake Anayoyapenda.

Kama mtoto wako anaonekana anapenda mpira mpe support, kama anataka kuimba mpe support kadri unavyoweza, maana hawa watoto huwa wanapenda kujaribu kila kitu kwa hiyo ukimpa support unampa chance ya yeye kujifunza kitu kwa undani na kuona kama anakiweza au la. Huwezi jua kesho yake atakwambia hataki tena kuimba kwa sababu amejaribu kwa nguvu zake na support yako ila hajapenda.

Jishirikishe Kwenye Mambo Yake ya Shule.

Nenda shule kaongee na walimu wanaomfundisha mtoto wako ili ujue anavyoendelea madhaifu yake na maeneo anayofanya vizuri. Kisha mwambie kuwa umeonana na mwalimu wake na umeona mapungufu gani kwake na umuulize ni wapi anataka umsaidie zaidi ili afanye vizuri. Angalia homework zake na kumsisitiza angalau ajaribu kumaliza homework zake mapema.

Mpongeze Kwa Tabia Zake Nzuri.

Tabia za watoto wa kiume huwa sometimes zinachanganya sana wazazi mpaka wakati mwingine unawaza ni jinsi gani ya kudeal na tabia hizo. ila sasa kama ukiona amefanya kitu kizuri au ameonyesha tabia nzuri basi hapo hapo mpongeze na kumjulisha kuwa umependa kitu alichokifanya na umekubali. Ukifanya hivyo unamuongezea hamu ya kuendelea kufanya mambo mazuri kwenye maisha yake.

LEAVE A REPLY