Kazi Ambazo Mtoto Anatakiwa Kufanya Kulingana na Umri Wake.

0
2749

Kazi Ambazo Mtoto Anatakiwa Kufanya Kulingana na Umri Wake.

Watoto Kadri wanavyokua wazazi huanza kuwafanyisha baadhi ya kazi mbali mbali na kuna wazazi wengine wala hawana muda wa kuwafanyisha kazi kwa kuona bado ni wadogo. Sasa ni kazi gani ambazo mtoto wako anatakiwa kuzifanya kulingana na umri wake? Zipo kazi nyingi ambazo mtoto anaweza kuzifanya cha muhimu ni kuangalia kazi unayotaka kumpa kama anaiweza mwenyewe au ni lazima na wewe uwepo chini ni baadhi tu kazi ambazo wanaweza kuzifanya….
Miaka 2-3
Mtoto wako akifikisha umri huu maswala ya kazi anakua anaweza kufanya kazi ndogo ndogo na kuwajibika. Kwa sababu yeye bado ni mdogo sio lazima kumfanyia kila kitu kuna baadhi ya vikazi ambavyo anaweza kufanya kama vile,
– Kutunza nguo zake chafu
– Kutunza midoli yake mahala pake
– Kutunza vitabu vyake
– Kutupa takataka

Miaka 4-7

Kadri mtoto anavyozidi kukua na uwezo wake wa kufanya kazi huwa unaongezeka hasa kama walikua wanakusaidia kabla ya kufikisha miaka 4. Kadri wanavyozidi kukua na kuanza kwenda pre school hizi ni baadhi ya kazi ambazo wanaweza kufanya
– Kurekekebisha meza ya kulia
– Kutandika kitanda
– Kumwagilia maji maua kama yapo nyumbani
– Kuosha vyombo
– Kufata vitu dukani ukimwagiza
– Kudeki sebuleni na usafi wa kawaida

Miaka 8-10
Watoto wanapofikia umri huu ratiba zao za kazi ndio huongezeka Zaidi kulingana na miaka yote ya chini waliyopitia. Vitu walivyosaidia kufanya kabla ya hapa wanaweza kuvifanya sasa kabisa wao peke yao bila hata ya wewe kuwepo na hapa wanaweza kuendelea kufanya kazi ambazo pia ni kwa ajili ya familia nzima sio vitu vyake tuu kama
– Kuandaaa meza ya chakula
– Kusafisha nyumba nzima ndani au nje kufagia
– Kuosha vyombo, kufua na hata kuosha gari
– Kusaidia kupika

Miaka 11 na Kuendelea
Baada ya mtoto wako kuanza shule ya msingi wanaanza kuwa wanataka kuwa free so hapa inamaanisha wanaweza kufanya mambo yao wenyewe bila ya wewe kuwepo. Kila mtoto anakua kivyake na kwa style yake lakini kuanzia miaka 11 na kuendelea kazi kama kufua ni kazi ambazo anatakiwa kuwa anazifanya kwa ufasaha zaidi na baadhi ya kazi zingine ni kama
– Kusafisha choo
– Kusafisha jikoni
– Kuosha vyombo
– Kufua nguo zake
– Kama ni wa day school anaweza kuweka chakula chake mwenyewe kwenye lunchbox
– Kufanya kazi ndogo ndogo za shamba au garden kupalilia
– Kuangalia wadogo zake wazazi wanapoondoka

Kila mtoto anakua kwa style yake na speed yake kuna baadhi ya watoto wanaweza kuanza hizi kazi mapema na wengine wanaweze kuchelewa ila hii ni inategemea na wewe mzazi wake kumuangalia umri wake na kuona ni kazi zipi anaweza kuifanya na baada ya hapo kadri anavyokua unazidi kumfundisha taratibu mpaka aelewe mwenyewe na kujitegemea mwenyewe mapema iwezekanavyo.
.

LEAVE A REPLY