Mambo Manne Kwanini Watoto Hutingisha Kichwa Kila Mara

0
4497

Mambo Manne Kwanini Watoto Hutingisha Kichwa Kila Mara

Umeshawahi kubeba watoto au kuona watoto wachanga na ukagundua kila mara huwa wanatingisha kichwa na hawatulii? Yaani muda aliotulia ni pale anapokuwa amelala ila akiwa macho ni kujitingisha mwanzo mwisho hii huwa ni nini? Kitu chochote ambacho mtoto atakifanya alafu hatukijui huwa kinatufanya tuogope na kuanza kuwaza ni nini tatizo. Mtoto akianza kutingisha kichwa gafla huwa inaogopesha na kuanza kuwaza kwanini anatingisha kichwa hivyo? Ila je kuna haja ya kuogopa kweli? Mambo manne ambayo unatakiwa kuyafahamu kuhusu hili swala….
So kama mtoto anatingisha kichwa kuna ulazima wa kuwa na hofu kuhusu tabia hii mpya au, labda ana kitu kinamsumbua.Tabia hii ya watoto kutingisha kichwa huwa ni ya kawaida na mara nyingi huwa inatokea mpaka wakati mwingine unamuona mtoto anajipiga mwenyewe kichwani na tumikono twake.

Sababu Kwa nini mtoto anajitingisha kichwa kila mara na ni wakati gani unatakiwa kuwa na hofu.
1. Watoto wengi wanaanza tabia ya kutingisha kichwa kama sehemu ya kujifunza jinsi ya kucontrol mwili wao. Wanakuwa wanakuigiliza unachokifanya au amegundua tu kuwa akijitingisha hivyo wewe unahudumia na kumpa attention kwa hiyo hapa hamna haja ya kuwa na hofu.
2. Watoto wengine huwa wanatingisha kichwa kama wakiwa wamechoka kwa hiyo ni kama anajipumzisha mwenyewe. Watoto wengine huwa wanatingisha kichwa mpaka wanapata usingizi na kulala. Hapa tena hamna haja ya kuwa na hofu ni wewe tu kumwangalia jinsi anavyo endelea.
3. Kutingisha kichwa mara nyingine mtoto anaweza kuwa anatatizo masikio. Kama mtoto wa anasikia baridi, au ana mafua au homa ni vema ukaenda kwa daktari. Watoto wakiwa na kitu kina wasumbua huwa wanatingisha kichwa labda sikio lake limeziba kwa hiyo anajaribu kulirekebisha kwa hiyo ni vema kumwangalia mapema.
4. Kitu kingine kwanini watoto hutingisha kichwa ni kwa sababu mbalimbali kama ana usingizi, au amejisaidia anataka kubadilishwa, kuna joto sana, au baridi sana au kuna kitu kinamsumbua na anaangaika mwenyewe kulitatua hilo tatizo kwa hiyo inabidi wewe kama mzazi kumwangalia na kumchunguza ni nini hasa kinaweza kuwa kinamtatiza na machoni ndio utajua kama ni sura ya furaha au ya maumivu.
Sasa iko hivi, mtoto akiwa mchanga kama mzazi una kazi kubwa ya kuwa mdadisi wa kuangalia na kuchunguza ni nin hasa kinamsumbua. Kina mama ambao huwa wanapata mtoto wa kwanza huwa wanapata shida sana kujua ni nini hasa mtoto anasumbuliwa, ila kwa wale ambao wanapata mtoto wa pili ndio wanaweza kujua, kwa hiyo kama ni mara yako ya kwanza kupata mtoto huna haja ya kuwa na wasiwasi sana.Mtoto akiwa anatingisha kichwa kila mara cha muhimu ni kumuangalia kama anafuraha usoni au la na ukiona sura sio ya furaha hapo sasa jaribu kuangalia kama kuna kitu kinamsumbua na uanze na kuangalia kama amejisaidia.

LEAVE A REPLY