Sheria 6 za familia ambazo wazazi wanatakiwa kuziweka.

0
1690

Sheria 6 za familia ambazo wazazi wanatakiwa kuziweka.

1. Kula Chakula Pamoja
Familia ambayo inakula chukula pamoja hukaa pamoja. Kula chakula pamoja huwa inasaidia wanafamilia kuwa karibu sana na kushare mambo yao ya siku nzima kwa pamoja. Ila sasa wakati wa kula kuna baadhi ya sheria ambazo unatakiwa kuweka
– Kula chakula kwenye meza ya kulia chakula na sio kwenye makochi
– Hakikisha tv inakua imezimwa wakati wa kula
– Wekeni simu mbali wakati wa kula
– Waambie watoto wawe wanaandaa meza kuweka sahani vijiko na maji
– Waambie watoto watulie na kula chakula badala ya kucheza, maana watoto wenyewe muda wa kula pia huwa wanaendelea kucheza kwa hali hii wakiendelea nayo wakikua itakua balaa.
– Waambie watoto wasiongee wakati wana chakula mdomoni.
– Tenga chakula mezani ambacho mnaweza kukimaliza, hii pia inamfundisha mtoto umuhimu wa chakula.
– Usiharakishe muda wa kula,kuleni taratibu maana huo ndio muda wenu wa kuongea na kubadlilishana mawazo wakati mnakula

2. Fata Sheria za Barabarani
Huwa ni bora kufika salama kuliko kubadilisha njia na kuelekea hospitali. Haijalishi una haraka kiasi gani ni vema ukafata sheria za barabarani na baadhi ya hizo sheria ni kama.
– Funga mkanda wote pamoja na watoto
– Hakikisha milango imefungwa
– Usiongee na simu wakati unaendesha
– Kama unasafiri na mtoto mdogo kabisa hakikisha amekaa vizuri au amebebwa na mtu vizuri
– Waambie watoto wako wasikusumbue au wsichezecheze kwenye gari wakati linatembea ni hatari.
– Waambie watoto wako wakusaidie kuangalia usalama wa barabara kama kuna mtu anaendesha vibaya wakukumbushe.

Hizi sheria ni vema mkazifata kila mara mnaposafiri kama familia. Sasa mara nyingi unakuta mama na baba ndio huwa wanafunga mkanda watoto wanawaaacha kwa kisingizio kwamba ni wadogo sio lazima, hiyo ni hatari kama mtoto amefikia umri wa kufunga mkanda afunge mapema.

3. Kuwa Wasitaarabu, Kuheshimiana, na Kupeana Company.
Kama mzazi hakikisha unaongea vizuri ukiwa na familia yako au ukiwa nje kazini au kwa majirani. Kumbuka point hizi
– Inaweza kuwa vigumu kuongea taratibu kama umekasirika lakini usiongee kwa nguvu na kupiga makelele hata iwe vipi. Jaribu kutuliza hasira kwanza kabla ya kuongelea hilo swala lililo kuudhi au vuta pumzi kwa nguvu alafu pumua taratibu mara kadhaa huwa inasaidia kupunguza hasira.
– Wafundishe watoto wako jinsi ya kuwa watulivu pindi wanapokuwa na hasira kama vile kuwapa muda watulie ili wamalize hasira zao.
– Waambie watoto uzuri wa maneno matatu muhimu. Samahani, Pole, Ahsante.Haya maneno yana umuhimu sana wakiweza kuyafahamu umuhimu wake yatawasaidia sana maishani mwao.
– Wasaidie kutumia muda wao kufanya kazi zingine ambazo zitawaondolea mawazo
– Njia nzuri ya kuwafusha watoto jinsi ya kuongea vizuri ni kwa kuwaonyesha mfano wa nyie wazazi kuongea vizuri. Wazazi ndio walimu wa kwanza kwa mtoto, kwa hiyo wakikuona unaongea vizuri na taratibu na wenyewe wanaweza kufata hiyo tabia maisha yao yote.
– Wafundishe watoto wako kuwaheshimu watu wazima, kuwatunza na kuwa nao karibu pale wanapowahitaji.

4. Fanyeni Kazi za Nyumbani kwa Pamoja
Huwa ni kazi mnapoamka asubuhi na unajikuta una kazi nyingi zinakusubiri wewe, jaribu kuwapa watoto kazi nao wafanye ili wakusaidie kupunguza mzigo.

– Mnapoamka asubuhi kusanyikeni hapo kidogo kwa dakika tatu mpangie ratiba kamili ya kazi kabla ya chai, mmoja aoshe vyombo, mwingine apike chai, mwingine afagie nje ili mradi msaidiane kazi za nyumba zipungue mapema.
– Tunza vitu maala pake kama funguo zijulikane zinakaa wapi na kila mmoja awe anajua, remote ya tv, sahani vijulikane sehemu yake.
Mara nyingi unakua kazi za asubuhi huwa watu wanazichukia ila kama unataka watoto wako waoenjoy hizi kazi wewe waambie tu kuanzia wanapoamka saa 12 asubuhi mpaka saa tatu wafanye kazi zao wanazotakiwa kufanya asubuhi baaada ya hapo kila mtu aendelee na shughuli zake.
5. Kuomba ruhusa na kuaga wakati wa kuondoka.
Unatakiwa kuweka mipaka na kuhakikisha kila mmoja anaifata. Baadhi ya mipaka hiyo ni kama
– Wafundishe watoto wako kuomba ruhusa kabla ya kuondoka
– Waambie wanaweza kwenda nje tu pale wanaporuhusiwa na mkubwa wao na kama wakiamua kubadilisha mahala pa kwenda wakutaarifu mapema.
– Hakikisha una namba za wazazi wa rafiki za watoto wako, maana wanaweza kusema wanaenda kwa kina Jose kumbe kaenda sehemu nyingine.
– Wape watoto namba zako za simu wanapoondoka
– Kama una watoto wadogo sana waambie waache kuongea ongea na watu wasio wafahamu.

6. Usafi
Usafi ni kitu kingine muhimu sana unatakiwa kuwaambia watoto wako juu ya swala la usafi kila mara unapoona wanafanya mambo ambayo yanahatarisha afya ya familia,
– Waambie waoshe mikono kabla ya kula na baada ya kula na baada ya kutoka uwani.
– Waambie watoto wako wawe wanafunika mdomo na pua wakati wanato chafya au wnapokohoa
– Waweke uchafu maala unapotakiwa kuwekwa
– Wanapoenda uwani wahakikishe wanakiacha kisafi kama walivyokikuta.

Yapo mengi ya kujifunza Ila haya ni 6 kwa leo.

LEAVE A REPLY