BAADHI YA SABABU KUBWA ZINAZOSABABISHA MTOTO MCHANGA KULIA USIKU

0
5164

1. Njaa

Mtoto akiwa na njaa na anahitaji chakula anaweza kulia ili kutaka shida yake itatuliwe. Lakini kwa bahati mbaya hana namna ya kukujulisha kuwa ana njaa zaidi ya kilio. Ni vyema kufahamu aina ya sauti ya kilio inayoashiria njaa. utajua hili kwa mazoea yako ya kila siku na mtoto wako.  Njaa ni mojawapo ya sababu kubwa kabisa ya mtoto mchanga kulia.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Mpe mtoto chakula kila mara kutokana na ulivyompangia. Kumbuka mtoto anakula kidogo na mara kwa mara.

Kama mtoto anaendelea kulia baada ya kula au anakataa chakula basi kutakuwa na sababu nyingine

 2. Joto au Baridi

Kama ilivyo kwa watu wazima,joto kali kupita kiasi au baridi inakufanya ujisikie vibaya na kutafuta jinsi ya kurekebisha kama vile kuvaa vazi zito kama kuna baridi au kuwasha feni au kiyoyozi,vivyo hivyo kwa mtoto mchanga, anahitaji kupata ubaridi kama kuna joto kali au kuvikwa nguo nzito ili apate joto kama kuna baridi

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Hakikisha mtoto anavaa nguo sahihi kulingana na hali ya hewa. Mpunguzie nguo au kufungua madirisha kama kuna hali ya joto.

Kama kuna baridi basi hakikisha unamvikanguo nzito mwilini ikiwemo miguuni na kichwani.

3. Uchovu na Usingizi

Watoto wanalia wakiwa na usingizi. Hii inatokea mara nyingi sana. Watoto wengi wana tabia ya kulia kabla ya kulala.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Fahamu kuwa mtoto anahitaji kulala muda mwingi sana inakadiriwa kuwa masaa yapatayo

Mtoto wa miezi 1-3: Masaa 15  (Mchana-5,Usiku-10)

Mtoto wa miezi 3-6: Masaa 14 (Mchana-4,Usiku-10)

Mtoto wa miezi 6-13: Masaa 12-14 (Mchana-3,Usiku-11)

Kama ukifahamu mtoto analia kwasababu ya usingizi au uchovu basi muogeshe na kumweka katika mazingira ya kulala(kumlaza mtoto)

Watoto wengine wanalala vizuri wakiwa wameshikwa mikononi na kuchezeshwa badala ya kitandani.

 4. Kubebwa na Kukumbatiwa

Watoto wanahitaji kubebwa na kukumbatiwa. Hii ni njia yaasili ya kunesha upendo kwa binadamu huyu mdogo.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Mtoto anapokuwa amelazwa kwa muda mrefu huwa anachoka na anahitaji kumbadirisha namna ya kulala napengine kubebwa mikononi na kukumbatiwa. Sauti   ya mapigo ya moyo ukimbeba kifuani kwako inamfanya ajisikie vizuri na kujiona anajaliwa.

5. Kubadirishwa Nepi

Mtoto anapojisaidia katika nguo zake anajisikia vibaya na kukosa uhuru.

Anahitaji kubadirishwa nepi,kuoshwa na kuvikwa upya

Mtoto akilia fikiria huenda amejisaidia na anahitaji kubadirisha nepi

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Mwangalie mtoto mara kwa mara kama amejisaidia na mbadirishe nepi zilizochafuka. Nepi zenhye mkojo au haja kubwa zinaweza kumsababishia mtoto kuungua ngozi hivyo ziondolewe kwa haraka.

6. Ugonjwa wa Tumbo na Maumivu Mengine

Watoto wachanga wanasumbuliwa sana na maumivu ya tumbo na wataalamu wanasema kuwa inaweza kusababishwa na chakula ambacho katika umri mchanga ni mziwa ya mama au maziwa ya bandia ambayo anapewa.

Soma:  Madhara ya Kupongeza Watoto-Kama unafikiri umekuwa ukifanya vyema basi fikiri tena.

Kwakuwa mfumo wake wa chakula bado ni mpya na unaendelea kukua basi unapata shida kumeng’enya chakula.

Inaaminika kuwa gesi inajaza tumbo na kusababisha maumivu kwa mtoto.

Njia ya Kukabiri Tatizo:

Shida hii si rahisi kukabiliana nayo na imekuwa ikiwapa wakati mgumu wazazi kwa watoto chini ya miezi 3.

Kumlaza mtoto kifudifudi iliatoe upepo ni njia mojawapo inayoshauriwa lakini katika usimamizi(Ni hatari kumlaza mtoto mchanga kifudifudi kwa kuwa anaweza akajiziba hewa na kusababisha kifo).

Kumshikashika tumbo kwa mikono au kitambaa chenye maji ya uvuguvugu inaweza ikasaidia kumtuliza.

Kuna dawa za kusaidia kulainisha utumbo wa mtoto na kutoa gesi. Tafadhari onana na daktari wa watoto upate ushauri zaidi.

Mwisho.

Mtoto anaelia anahitaji msaada na anatoa mawasiliano kuwa ana shida. Kwakuwa hawezi kusema wala kuonesha ni nini unahitaji kuangalia mambo yote ya msingi kama yalivyotajwa ilikujua anasumbuliwa na nini.

Ugonjwa tumbo unachangamoto kubwa zaidi kukabiliana nao na kwa kweli unawasumbua watoto wengi na wazazi pia kwa kuwa hakuna kikubwa ambacho uaweza kufanya kuondoa maumivu kwa mtoto wako. Hata hivyo bado mbinu zilizotajwa zinaweza kusaidia kukabiriana na matatizo yanayosababisha mtoto mchanga kulia usiku.

LEAVE A REPLY