Kuhusu Mtoto Magazine

IMG_8112Tovuti hili ipo kukusaidia kupata masomo, mafunzo, ujuzi, uelewa, elimu katika swala zima la malezi. Wanasema kulea mimba si kazi kazi kulea mwana. Kwa maana ishu ya kumlea mtoto mpaka akue si kazi ndogo. Na malezi sio peke yako utakuta jamii nzima inahusika katika kumlea mtoto wako. Kuna vitu utakuwa hujui lakini utapata mafunzo kutoka kwa mwingine.

Wazazi watatusafirisha katika simulizi za watoto wao na namna wamebadili maisha yao. Tutaanza na mimi na mwanangu Zion ambae yeye ndio sababu kubwa ya mimi kuanzisha tovuti hii.

Wazazi ndio mhimili mkubwa wa maisha ya mtoto katika kumlea, kumuongoza, kumlinda, kumfundisha na kumhudumia. Mtoto huleta faraja na matumaini kwa mzazi ndio maana wazazi hufanya kila wawezalo ili mtoto akue vyema. Kama unatafuta namna ya kuweza kukamilisha hayo karibu sana tujifunze pamoja.

Toka nimejaaliwa kuwa mama wa Zion maisha yangu yamebadilika kwa kiasi kikubwa. Kuna msemo upo siku nyingi kwamba mtoto huja na baraka, na zamani wazee wetu walizaa watoto wengi wakiamini kila mtoto huja na baraka zake. Mtoto wangu amenifanya niwaze zaidi na niishi pia katika dunia yake ya utoto. Nishiriki na wakina mama na wazazi wengine katika dunia hii ya watoto.

Nilipopata mtoto tu nikaanza kufikiri namna nitakavyoshiriki na kina mama wengine. Wakati nikifurahia maisha haya mapya ya kuwa mama pia nishiriki kwa kufurahi, kusherehekea, kuelimisha na kuzungumza na wakina mama. Ndio nikawaza kuwa na jarida na tovuti hii ili tusome na iwe msaada kwetu katika safari hii ya malezi ya watoto wetu.
Naamini harakati hizi zitagusa wazazi wengi na hasa wazazi wapya.